Breaking News

Jeshi la Uganda lakana madai ya kutaka kuisaidia Kenya

Na Yahya masangula

Jeshi la  Uganda la UPDF limekanusha taarifa kuwa liko tayari kuingia nchini Kenya kusaidia kudhibiti hali ya usalama nchini humo baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu juma lililopita.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, huku mpinzani wake mkuu Raila Odinga akiyapinga matokeo hayo.

Waziri wa mawasiliano wa nchini humo, Frank Tumwebaze amesema jeshi la Uganda haliwezi kutumwa nje kushiriki operesheni ya kijeshi kisiri.

Msemaji wa jeshi hilo, Richard Karemire, kupitia taarifa yake, amesema Kenya ni nchi huru na usalama wake uko chini ya serikali ya nchi hiyo.

Aidha, amesema Uganda haijapokea ombi kutoka Kenya kutuma majeshi yake nchini humo au kuomba usaidizi.

No comments