Breaking News

Mbunge awajulia hali majeruhi ajali ya lori

Baadhi ya majeruhi hali zao zinaelezwa kuwa  mbaya kutokana na kuvunjika viungo mbalimbali mwilini.

Singida. Mbunge wa Viti Maalumu, Aysha-Rose Matembe amewatembelea na kuwajulia hali majeruhi 20 wa ajali ya lori lililokuwa limewabeba wafanyabiashara kutoka mnadani kwenye Kijiji cha Mtinko kwenda Singida Mjini.

Katika ajali hiyo iliyotokea juzi Agosti 27, watu sita walipoteza maisha na wengine 42 walijeruhiwa.

Matembe aliwatembelea na kuwajulia hali majeruhi hao waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa Singida.

Mbunge Matembe amewahimiza madaktari kuendelea kuwapatia huduma za haraka ili kuokoa maisha yao.

Mbunge huyo pia amewatembelea wafiwa waliopoteza ndugu na jamaa kwenye ajali hiyo ili kuwafariji.

Ameliomba Jeshi la Polisi kuimarisha ukaguzi wa magari na madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani kama mkakati wa kwanza wa kukabiliana na ajali zinazosababisha vifo na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

No comments