Bulaya kumpeleka Wasira mahakamani
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara, Ester Bulaya amesema amepanga kudai fidia dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa mwaka 2015, Stephen Wasira baada ya kumshinda katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
Bulaya ametoa msimamo huo baada ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo kutaka kujua endapo atamsamehe Stephen Wasira au la.
“Tukitoka hapa, tunaenda mahakamani kudai fidia yetu, tulete maendeleo katika jimbo la Bunda Mjini”. Amesema Bulaya
Kuhusu utatuzi wa kero ya maji jimboni humo, Bulaya amesema ametenga shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununu mabomba katika kata SABA za jimbo hilo.
No comments