Zambia yaikamia Taifa Stars Cosafa
Afrika Kusini. Timu ya Zambia inashuka dimbani kesho Jumatano kukabiliana na Taifa Stars kwenye mchezo wa nusu fainali unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.
Mchezo huo utapigwa mjini Rustenburg, Afrika Kusini huku Kocha Wedson Nyirenda akisisitiza kuwa, kikosi chake cha Chipolopolo kina matumaini ya kuibuka na ushindi.
Katika mechi mbili kabla ya mashindano hayo, timu hiyo hiyo ilipoteza mchezo mbele ya Msumbiji kwa kufungwa bao 1-0 wakati wa mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) na nyingine ikaifunga Afrika Kusini kwenye mechi ya kirafiki.
Hata hivyo, katika mashindano ya Cosafa walishinda mabao 2- 1 dhidi ya Botswana mchezo uliopigwa juzi Jumapili.
Zambia watashuka Uwanjani wakimtegemea mshambuliajia wao, Donashano Malama.
No comments