SPORTPESA SI MCHEZO, SASA YATINGA NCHINI ITALIA KWA KISHINDO
Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa imetangaza rasmi kuwa imefanikiwa kupata hisa za umiliki wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya RCS ya nchini Italia ambayo inamilikiwa na kampuni mama ya RCS Media Group.
Shughuli za sasa za uendeshaji za kampuni hiyo zimekuwa zikifanywa chini ya usimamizi wa nembo ya GazzaBet huko nchini Italia ikiwa ni miaka mitatu sasa ambapo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliteka soko la michezo ya kubashiri la nchini humo.
“Hii ni hatua nyingine kubwa katika harakati za kuendelea kuifanya SportPesa kuwa kampuni kubwa duniani. Kupata hisa kwenye kampuni ya michezo ya kubashiri ya RCS kutawezesha kampuni kukua kwa kasi nchini Italia na itatoa fursa mpya kwetu kutangaza utamaduni wetu kama SportPesa kwa wateja wetu wa sasa na wa baadae”, alisema Adam Beighton, Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya SportPesa nchini Italia.
Akizungumzia kuhusu hili, Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa nchini Tanzania Ndugu Pavel Slavkov alisema kuwa kuongezeka kwa Italia kwenye orodha ya masoko yao ya kibiashara ni mafanikio makubwa kwao kama kampuni.
“SportPesa ina furaha kubwa kutanua wigo wake kibiashara katika nchi ya Italia ambayo imekuwa ni soko kubwa la michezo ya kubashiri barani Ulaya. Kuiongeza Italia kwenye orodha yake ya utendaji ni mafanikio makubwa huku tukitazamia kuboresha huduma kwa wateja wetu waliomo nchini humo na kuzifanya kuwa za kiwango cha daraja la juu zaidi”, alisisitiza Ndugu Pavel Slavkov.
RCS Media Group wataendelea kuwa wamiliki wa hisa wa kampuni hiyo kwa asilimia chache huku wakiwa na shauku kubwa ya kuona jinsi ambavyo fursa hiyo itatanua wigo wa kampuni hiyo kibiashara.
No comments