Breaking News

Serikali kupeleka maji safi na salama Mbagala na Temeke


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ina ahadi kutoka Benki ya Dunia ili kuweza kuweka miundo mbinu ya usambazaji wa maji ili kuhakikisha Temeke na Mbagala yanapata maji safi.


Mhandisi Kamwelwe amesema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Temeke Abdallah Mtolea, leo bungeni mjini Dodoma lililohoji,

Wananchi wa Temeke si wanufaika wa maji yanayotoka mto Ruvu hivyo hatuna mfumo wa mabomba tunatumia maji ya Kisima, Je serikali ina mpango gani wa muda mfupi wa kutuletea maji safi ili tuache kutumia maji machafu?


“Temeke kwanza tunao mtambo wa maji wa mtoni ila kweli maji yanayotoka pale ni machache, lakini bado tunakamilisha uchimbaji wa visima 20 Kimbiji na Mpera, na sasa hivi tunapeleka fedha na tuna ahadi kutoka Benki ya Dunia ili tuweze kuweka miundo mbinu ya usambazaji kuhakikisha kwamba maeneo yote yale Mheshimiwa mbunge Temeke na Mbagala yaweze kupata maji safi na salama. kwahiyo ni suala la wakati tu tayari maji tunayo kwahiyo ni fedha tu ili wananchi wako waweze kupata maji safi na salama,” amesema Mhandisi Kamwelwe.

No comments