Breaking News

NDEMLA AONGEZWA KIKOSI CHA TAIFA

Kocha Mkuu wa kikosi cha Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' Salum Mayanga amemjumuisha kiungo wa kikosi cha Simba Said Ndemla katika orodha ya wachezaji aliowataja kwenda kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Rwanda kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN). Mchezo huu utafanyika tarehe 15.7.2017 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

 

Ndemla anakwenda kwenye kikosi hicho ambacho ataungana na wachezaji kutoka katika vilabu mbalimbali ambapo kutoka katika klabu ya Simba ni (Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Salim Mbonde, John Bocco)

 

Hakikisha ume-Update Simba App yako kuweza kuangalia Simba Exclusive, kusoma Sauti ya Simba, Kupakua picha muhimu, pamoja na kupata habari rasmi za usajili. 


No comments