Breaking News

MWANJARI; NIKO FITI WATAISOMA NAMBA


SIMBA inaendelea kujifua kwa nguvu kwa ajili ya msimu ujao huko nchini Afrika Kusini, ambapo habari nzuri kwa mashabiki wa timu hiyo kwa sasa ni kurejea kwa beki wao tegemeo, Method Mwanjali.

Mwanjali ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu na kushindwa kuitumikia timu hiyo mzunguko wa pili wote, kwa sasa amerejea na yupo na timu hiyo nchini Afrika Kusini.
Beki huyo kutoka Zimbabwe akiwa na sifa ya vitu vingi uwanjani, anacheza kwa kutumia nguvu na akili, hana makosa ya kizembe kurejea kwake inaweza kuwa habari nzuri sana kwa mashabiki wa Simba kwa sasa.

Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, alisema kambi yao nchini humo inakwenda vema ikiwa sambamba na Mwanjali ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa nje.

“Mazoezi yanaendelea vema na tunafanya mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, wachezaji wote wapo vema nina imani kambi hii itaweza kutusaidia,” alisema.

Akizungumzia hali ya baridi nchini Afrika Kusini, Omog alisema hali hiyo haiwezi kuwaathiri lolote kwani wanaendelea na mazoezi kama kawaida.

“Maandalizi yanaendelea vema na hali ya hewa haiwezi kutuzuia tushindwe kufanya mazoezi vizuri ambapo kwa wiki hii yote tutakuwa tukifanya peke yetu kabla ya kutafuta mchezo wa kirafiki,” alisema.

Simba ipo Afrika Kusini kwa siku ya tatu sasa ikijiwinda na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara sambamba na kujiandaa na tamasha lao la kila mwaka la Simba Day linalofanyika Agosti 8 ya kila mwaka.

Pamoja

No comments