Mwanachuo aliyeshtakiwa kwa makosa ya mtandao aachiwa huru
KISUTU: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachilia huru Jovenary Shirima ambaye ni mwanafunzi wa Chuo mjini Arusha aliyekamatwa tangu mwezi Januari mwaka huu akituhumiwa kwa makosa ya mtandao.
Akizungumza mara baada baada ya kuachiliwa huru, wakili wa Shirima ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema tangu hiyo ufunguliwe upande wa walalamikaji hawakuweza kuendelea kuhudhuria mahakamani jambo lililopelekea kufutwa kwa kesi hiyo.
“Walalamikaji wameikacha kesi kama walivyokacha walalamikaji wa kesi ya Mbunge wa Arsuha Mjini, Godbless Lema”.
No comments