Mkusanyiko usio halali wawaponza viongozi Chadema
Mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora juzi iliwahukumu kwenda jela viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Viongozi hao wamehukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko usio halali.

Waliohukumiwa kwenda jelakila mmoja kwa mwaka mmoja ni diwani wa zamani wa Igunga, Vincent Kamanga (52) ambaye kwa sasa ni Katibu wa Uenezi wa chama hicho wilayani hapa.
Mwingine ni Fea Rifa (41), Mwenyekiti wa Chadema Tawi la Mwamsunga na Luhanya Zogoma (48), Katibu wa chama hicho Tawi la Mwamsunga katika Kijiji cha Mgongoro.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elimajid Kweyamba mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ajali Milanzi alidai kuwa Oktoba 30, mwaka jana kati ya saa nne asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika Kitongoji cha Mwamsunga, washtakiwa wakiwa wafuasi na viongozi wa Chadema wakiwa na nia ovu, walifanya mkusanyiko usio halali. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Milanzi alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umewaona washitakiwa wana hatia hivyo, kila mmoja atatumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela huku akimuachia huru mshtakiwa wan ne, Idd Athumani.
Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi
No comments