Breaking News

Mkimuona Rooney pale taifa keshokutwa mpeni hii barua yangu

Hello Wayne!Nataka nikuambie kitu kwamba sikuwahi kuamini kama baada ya kizazi cha wakina Andy Cole na Dwight Yorke sikuamini kutatokea mchezaji mwingine Manchester United ambaye nitampenda kama nilivyowapenda wachezaji hao lakini wewe ulinisahaulisha kuhusu enzi zao.

Ulipokuja kutoka Everton sikuwa nakuamini na nilidhani umekuja tu kula hela na kuondoka kama wafanyavyo wengine, lakini September 28 mwaka 2004 ulinistaajabisha na kuniacha nikishangaa uwezo wako na umri wako.

Ile hattrick yako zidi ya Fernabache katika mchezo wa UEFA ilitufanya utuibie mioyo yetu mashabiki wengi wa Manchester United na wote tukaanza kununua jezi zako tukipita mtaani kifua mbele na kuimba jina lako “OUR BLACK PELE”

Kumekuja watu wengi United toka nianze kukupenda,wamekuja wengi na kuondoka ila wewe hukutaka kutuacha peke yetu ulikomaa na sisi kipindi cha shida na raha, ulikaa na sisi kipindi tukiwa namba na ulikaa na sisi kipindi tukiwa namba moja,We Thank You Wazza.

Roho inauma kusema kwaheri,roho inauma kutokukuona tena ukivaa jezi yetu na ukiwafunga Man City mabao yaliyokuwa yanawaumiza sana huku yakitufanya tucheke kwa furaha jinsi ulivyokuwa unawaadhibu wapinzani wetu.

Naamini unarudi nyumbani, unarudi sehemu uliyokulia,unarudi kukutana na marafiki zako ila asante sana kwa yote uliyotufanyia, WE THANK YOU FOR THE MEMORIES AND WE WISH YOU ALL THE BEST WAZZA.

No comments