Breaking News

Miswada ya sheria yazua mapya bungeni

Mbunge wa Arusha mjini, Godblss Lema akichangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi  kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka 2017.Picha na Emmanuel Herman 

Kwa ufupi

Wabunge wasema miswada hiyo haizungumzii madini tu, bali maliasili zote

By Sharon Sauwa, Mwananchi Ssauwa@mwananchi.co.tz

Dodoma. Wakati miswada miwili ya sheria zinazohusiana na umiliki wa maliasili, ikijadiliwa jana, vijembe na kurushiana maneno kati ya wabunge vilitawala.

Miswada hiyo ni wa Sheria ya Mapitio Majadiliano kuhusu Masharti hasi katika Mikataba ya Maliasili za nchi wa mwaka 2017 na Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa mwaka wa Fedha 2017.

Akichangia katika mjadala huo, Mbunge wa Vwawa, (CCM) Josephath Asunga amesema katika miswada hiyo hawazungumzi madini tu bali maliasili zote zilizopo nchini.

 “Hatuwezi kusubiri tuwe na muda wa kutosha kwasababu tumeibiwa vya kutosha, maliasili zimeibiwa kwa muda mrefu, lazima kwa wakati huu tunaanzia hapa kama kutakuwa na mapungufu tutaendelea kuya shughulikia,”amesema.

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Emmanuel Mwakasaka amesema wakati Serikali ikibana kuibiwa kwa rasilimali za Taifa kwa usimamizi madhubuti, wapinzani wanasema wasiwe wanabana moja kwa moja.

Hatua hiyo ilimfanya Mbunge wa Momba (Chadema) kuomba kutoa taarifa lakini Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alikataa akisema kitakachoruhusiwa wakati wa mjadala ni kuhusu utaratibu tu na si kingine.

Hatua hiyo ilizua minongongo miongoni mwa wabunge wa kambi ya upinzani jambo lilomkera Dk Tulia.

“Kwanini hamjifunzi mkiambiwa mnazomea kwa sababu gani mnazomea? Alihoji Dk Tulia.

Lakini Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche ameomba utaratibu na kutumia kanuni ya 64 akisema kwamba Mwakasaka amesema uongo.

Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika amesema kila asubuhi wamekuwa wakisali bungeni ili haki itendeke lakini haki haitendeki.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi , Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama ameomba utaratibu kwa kutumia kanuni ya 64 (1D na G).

No comments