Breaking News

Mdee ataka halmashauri wanazoshikilia kusomesha waliopata mimba shuleni

Mdee ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wake aliofanyia makao makuu ya  Chadema jijini hapa

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema(Bawacha), Halima Mdee amezitaka halmashauri zinazoongozwa na chama hicho kuhakikisha zinawasaidia waliopata mimba shuleni kuendelea na masomo.

Mdee ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wake aliofanyia makao makuu ya  Chadema jijini hapa.

Amesema viongozi wa halmashauri hizo hawapaswi kuogopa kutimiza wajibu wao kutokana na kauli ya Rais John Magufuli  ya kuzuia wanafunzi wanaopata mimba kutoendelea na masomo.

Alisema wenyeviti wa halmashauri zilizopo chini ya Chadema waonyeshe  mfano kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi Katiba na sheria  ikiwamo ya elimu ambapo pamoja na mambo mengine inaweka misingi ya kupata elimu na kutobaguliwa kwa  kigezo  chochote.

"Nafahamu Rais anachukia  wanawake, ana mfumo dume  hii imeonyesha kwenye uteuzi wake, ila sikujua kama anawachukia hadi wasichana yaani msichana akipata mimba shule ndoto zake zinazimwa, wengine walibakwa,"alisema Mdee.

No comments