Breaking News

MAYWETAHER AMWAGIA DOLA MCGREGOR, ILA MAJIBU ALIYOPEWA HANA HAMU!

BONDIA Floyd Mayweather usiku wa jana alimwagia noti za dola za Kimarekani mpinzani wake, Conor McGregor katika mwendelezo wa promosheni ya pambano lao Agosti 26, mwaka huu.

Katika mkutano huo wa tatu kuwakutanisha uso kwa uso kwa ajili ya ziara ya promo la pambano lao, Mayweather alimuita McGregor muachaji akimanisha hawezi kuvumilia kumalizia jambo na kisha akamrushia noti za dola akisema; "Naendesha shoo, hi ni** yangu na na ninamwagia dola moja huyu****."

Baada ya siku tatu za promosheni, baadhi wamesema wawili hao wanakwenda nje ya mstari, wakati pia wawili hao wameshindwa kuheshimiana.Bondia Floyd Mayweather akijivuta pembeni baada ya kumwagia dola mpinzani wake, Conor McGregor usiku wa jana
Wakati wawili hao waliibuka watulivu safari hii, hakukuwa na msisimko hadi Mayweather aliposogea jukwaani na 'kulianzisha'. 

McGregor alimkandia Mayweather "uso kwa uso" mwanzoni kwa kumuambia anaelekea kufilisika kama rafiki yake '50 Cent'. "Amefilisika na wewe unaelekea.'

Nyota huyo wa Ireland kisha akampa Mayweather albamu mpya ya Jay Z na kumuambia ampe 50 na amuambie 'blanco amekutumia'. 

"Hawajui mimi ni nusu mweusi? Mimi ni nusu mweusi haswa," alisema ili kujikosha na tuhuma za ubaguzi wa rangi alizokwishaanza kutupiwa na kwenda kucheza na shabiki wake wa kike mweusi.

Baadaye Mayweather akakamata kipaza sauti tena na kusema: "Unajua nini, ninakuka? ninanuka****'.

Kisha akaugeukia umati kuuambia umnyooshee kidole 'muachaji' kabla mistari ya wimbo 'Baby Tap Out' haijaanza kusikika kwenye spika kubwa. 

Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 40 kisha akaanza kumtupia noti za dola McGregor ambaye alijibu kwa mshituko: "Zote ni dola moja moja! Ziko wapi fedha halisi?'

"Kwa sababu huo ndiyo utajiri wako wote," Mayweather akakasirika.

Mmarekani huyo kisha akaonekana kutaka kumvaa mpinzani wake, kabla ya timu yake kumuondoa McGregor. Timu ya bondia wa Ireland inayowahusisha Dillon Danis na Owen Roddy, nayo haraka ikaingia, huku umati wa 19,000 uliokuwepo ukumbini ukishangilia.

Upinzani wao utaendelea Uwanja wa Wembley mjini London, Ijumaa jioni. 

No comments