Majaliwa Amkalia kooni Mkurugenzi Lindi
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Lindi, Samuel Warioba Gunzar leo alijikuta katika wakati mgumu mbele ya waziri mkuu wa Jamuhuri ya Tanzania, Kassim Majaliwa baada ya kukutana na maswali mzito mfululizo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa nchi.
Hayo yamejiri katika mji mdogo wa Mtama kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa umefurika mamia ya wananchi. Hali ilikuwa mbaya kwa Gunzar kutokana na taarifa iliyotolewa na mbuge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye aliyekueleza waziri mkuu kwamba katika mji huo mdogo in unaokadiriwa kuwa na wakazi takribani 4000 hauna kituo cha afya.
Maelezo ya Nape yalisababisha waziri mkuu amuite mkurugenzi huyo aeleze nikwanini eneo hilo lisiwe na kituo cha afya wakati linaidadi kubwa ya watu. Huku akihoji kwanini imekuwa hivyo wakati kuna madiwani na watendaji katika halmashauri hiyo.
Alisema sera ya afya ipo wazi nasifa za kuwa na zahanati, vituo vya afya na hospitali zinafahamika. "Mkurugenzi njoo utueleze kwanini hapa hapana kituo cha afya na mipango ya halmashauri ni nini katika kushugulikia tatizo hili ambalo kimsingi limehusisha uhai na maisha ya wananchi," alianza kushusha maswali Majaliwa. Gunzar alijibu kuwa wanalifahamu tatizo hilo, bali mchakato wa kushugulikia unaendelea. Jibu ambalo waziri mkuu hakuridhishwa nalo.
Badala yake bila kuchelewa aliuliza na kutaka kujua maana ya maneno mchakato, tumekichukua na tutafanyia kazi. "Mchakato maana yake nini, mlikuwa hamjui na mlijipangaje huko nyuma kushugulikia jambo hili na juhudi gani zilifanyika, sitaki kusikia mambo ya mchakato. Wananchi wanahitaji kuhudumiwa na serikali yao ili wafanye shuguli za maendeleo.
Niambie hapa mlijipangaje na mlianza kutanga shilingi ngapi kama halmashauri ," alihoji Majaliwa. Hata hivyo badala ya kujibu maswali hayo mkurugenzi huyo alisema "Kwakuwa serikali yenu inasikiliza kero za wananchi na kwa kuangalia umati huu nalichukua mheshimiwa waziri mkuu, " Gunzar alisema huku akitweta. Kama hiyo haikutosha, Waziri mkuu alimuuliza swali la haraka:"Serikali yao, nawewe serikali yako yepi, " Gunzar alilazimika kubadilisha kauli na kusema serikali yetu.
Hata hivyo haikuwa mwisho wa mchezo. Kwani waziri mkuu aligeukia ujenzi wa kituo cha mabasi ambao hauleweki utakwisha lini. Alimtaka mkurugenzi aeleze sababu zakutokamilika ujenzi huo. Hata hivyo majibu aliyopewa hayakumridhisha kwa mara nyingine. Alisema kumekuwa na tabia ya kuwadanganya wananchi na viongozi katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
"Mkianza vikao na wananchi wakianza kuhoji mnaleta kifusi tripu moja, mkisikia waziri mkuu anakuja mnaleta makatapila, mmepeleka katapila pale kwa ajili yangu. Nikiondoka mtaondoa. Sasa lile halitoki, kama mlileta lifanye kazi basi lifanye.
Kama mlikuwa mnapiga, basi imekula kwenu safari hii. Lile halitoki hadi mumalize ujenzi nanitafuatilia kwa karibu,"alionya na kutahadharisha. Waziri mkuu Majaliwa alisema watumishi wa umma nilazima watimize wajibu wao wa kuwatumikia wananchi na kuachana na tabia za ubabaishaiji.
Kwasababu serikali ya awamu ya tano haina nafasi ya watumishi wa aina hiyo. "Muda wakuwababaisha, kuwasumbua na kuwazuga wananchi umekwisha. Ukiona huwezi kaa pembeni kwa hiari yako badala ya kusubiri kuondolewa kwani nilazima utaondolewa," alisema Majaliwa. Alisema serikali imekusudia kujenga uaminifu, uadilifu na nidhamu kwa watumishi.
Hivyo haitaki kuona watumishi wanafanya mambo ya ovyo. Alifafanua kuwa baada ya kuweka mikakati mazuri ya kukusanya na kudhibiti matumizi ya ovyo ya fedha za umma. Ikiwamo kusimamia vizuri ulipaji kodi, kupambana na rushwa na ufisadi mapato yameongezeka. Kwahiyo ni muda muhafaka wakupeleka huduma bora kwa wenye nchi. Huku akionya kuwa fedha zitakazo tolewa kwa shuguli zinazohusu maendeleo ziende zilikokusudiwa. Vinginevyo zinaweza kuwatokea puani watakao jaribu kubadilisha matumizi au kuzichezea. Majaliwa amehitimisha leo ziara yake ya siku nne mkoani humu. Baada ya kutembelea wilaya za Liwale, Ruangwa na Liwale. MWISHO.
No comments