Liverpool yamtolea Jicho beki wa Arsenal
Klabu ya Liverpool imetangaza nia yake ya kumsajili beki wa kulia wa Arsenal, Kieran Gibbs katika msimu huu wa usajili wa kiangazi.
Beki hiyo anayesakwa na Kocha Jurgen Klopp anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wanne waliopo kwenye orodha ya kusajiliwa klabuni hapo.
Gibbs mwenye miaka 27 ana uzoefu wa kutosha na amekuwa beki imara jambo ambalo linawafanya Liverpool kukosa usingizi kwa ajili ya kuidaka saini yake.
Liverpool wameamua kujitosa kwa mchezaji huyo, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwakani.
No comments