Kwa mara ya kwanza Ujerumani watwaa Confedaration Cup
Kabla ya mchezo wa fainali kati ya Ujerumani waliokuwa wakiikabili timu ya taifa ya Chile kulikuwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Mexico na Ureno.
Katika mchezo wa mshindi wa tatu magoli kutoka kwa Pepe na Adrien Silva yaliifanya Ureno kuibuka na ushindi wa mabak mawili kwa moja huku lile la Mexico likitokana na kujifunga kwa mlinzi wa Ureno Neto.
Baadae kulikuwa na mchezo wenyewe sasa wa fainali ambapo mabingwa wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani walikuwa wakikabiliana na mabingwa wa Copa America timu ya taifa ya Chile.
Bao la dakika ya 20 la Larsi Stindl liimaliza kabisa Chile na kuwafanya Ujerumani kubeba ubingwa wa michuano ya Confederation Cup kwa mara ya kwanza.
Chile walionekana kupambana sana kutaka kusawazisha bao hilo na juhudi za mlinda lango wa Ujerumani Adre Ter Stegen ulikuwa kikwazo kikubwa kwa Chile.
Timu ya taifa ya Ujerumani ambayo imeenda safari hii ikiwa na wachezaji vijana wengi wanachukua kombe hilo kutoka kwa Brazil ambao ndio walikuwa wanalishikilia.
Kivutio kikubwa katika mchezo huo ilikuwa uwepo wa wacheza soka wakubwa wa zamani Diego Maradona wa Argentina na Ronaldo De Lima wa Brazil ambao walikuwa uwanjani kushuhudia fainali hiyo.
No comments