Kigogo Escrow adaiwa ana uvimbe kama puto
Seth, ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Pan African Power Solution, ameshtakiwa na mfanyabiashara mwingine maarufu nchini, James Rugemalira kwa kuhujumu uchumi kutokana na ushiriki wao katika sakata la uchotwaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow lililohusu kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Dar es Salaam. Wakili wa washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha ameiambia mahakama kuwa mteja wake, Harbinder Sing Sethi hajalala usingizi kwa wiki nne kutokana na kusumbuliwa na uvimbe unaofanana na puto.
Seth, ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Pan African Power Solution, ameshtakiwa na mfanyabiashara mwingine maarufu nchini, James Rugemalira kwa kuhujumu uchumi kutokana na ushiriki wao katika sakata la uchotwaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow lililohusu kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Kutokana na kesi yao kutokuwa na dhamana, wawili hao wako mahabusi ya Keko.
Wakili Alex Balomi anayemwakilisha Sethi alidai hali ya mteja wake imeendelea kuwa mbaya na kwamb, hajapata usingizi kwa takriban wiki nne.
Alisema hayo baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kuieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Baada ya kusikiliza pande hizo mbili, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi aliagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha linawasiliana na wataalamu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kila inapobidi ili kuhakikisha afya ya mshtakiwa inakuwa nzuri na anapohitajika mahakamani afike.
No comments