Breaking News

Acacia, Geita zakubali kutekeleza sheria

Wakati Ashanti ikiwa na msimamo huo, Kampuni ya Acacia imesema ipo tayari kuanza kulipa asilimia sita ya tozo ya mrabaha, kiasi kipya kilichowekwa na sheria mpya iliyoanza kutumika mwaka huu wa fedha wa 2017/18.

Dar es Salaam. Wiki mbili baada ya Bunge kupitisha miswada ya mabadiliko ya sheria za madini, Kampuni ya AngloGold Ashanti inayoendesha Mgodi wa Geita, imesema itafanya mazungumzo na Serikali ili kulinda masilahi yake.

Wakati Ashanti ikiwa na msimamo huo, Kampuni ya Acacia imesema ipo tayari kuanza kulipa asilimia sita ya tozo ya mrabaha, kiasi kipya kilichowekwa na sheria mpya iliyoanza kutumika mwaka huu wa fedha wa 2017/18.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, AngloGold Ashanti inayomiliki kampuni tanzu za Samax Resources na Geita Gold Mining (GGM) inayoendesha Mgodi wa Geita, imesema itafanya mazungumzo hayo ili kuhakikisha GGM haiathiriki na mabadiliko hayo ya sheria.

“Sheria zote tatu zimefanya mabadiliko kwenye uchimbaji wa madini, mafuta na gesi. Kampuni yetu inachukua hatua za makusudi kuhakikisha inalinda masilahi yake kwa mujibu wa mkataba (MDA) uliopo kwa kuanzisha majadiliano chini ya Sheria za Biashara za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa,” inasema taarifa hiyo.

 Kama ilivyokuwa mwanzo, Acacia imekuwa ya kwanza kusema ipo tayari kulipa.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Acacia imesema inatambua kupitishwa kwa sheria mpya na kutekeleza matakwa ya mabadiliko ya sheria mbalimbali.

No comments