Breaking News

KESI YA MANJI YAAHIRISHWA, AENDELEA KUTIBIWA MUHIMBILI


Yusuf Manji.

 KESI inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jiji Dar hadi Agosti 4 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

Kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu, Huruma Shaidi ilikuwa isikilizwe leo lakini Manji hakufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa na mawakili wake kuwa ni mgonjwa na yupo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Muhimbili akitibiwa maradhi ya moyo.

 

Julai 5 mwaka huu, Manji akiwa amelazwa Muhimbili alisomewa mashtaka saba na watuhumiwa wenzake, yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, waMkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogweplate number mbili za magari ya serikali jambo ambalo nalo ni kinyume cha sheria.

Watuhumiwa wengine katika sakata hilo niDeogratius Kasinda na Thobias Pwere na mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja na wote wamerudishwa rumande.

No comments