Hakuna atakae baki salama mapambano ya dawa za kulevya – Mh. Masauni
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa wito kwa wananchi na wageni kuacha kujihusisha na biashara haramu ya madawa kwa kuwa hakuna atakae baki salama kwenye mapambano hayo.
Hayo yameelezwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Faharia Hamisi aliyehoji;
Mara nyingi kumekuwa na taarifa za watumiaji wa dawa za kulevya kwenye maneno mbalimbali nchini baada ya kukamatwa ni nini kinaendelea?
“Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali katika kudhibiti dawa za kulevya mashambani na viwandani hatua hizo zinadhibiti kilimo cha bangi uingizaji usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya kote nchini, kwa kuwakamata watuhumiwa na kuwapeleka katika vyombo vya sheria katika kipindi cha kuanzia Octoba 2015 mpaka 2017, Jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiaji mbalimbali ambapo watuhumiwa takribani 14,748 kesi zao zinaendelea Mahakamani ,Watuhumiwa zaidi ya 2000 walipatikana na hatia wakati watuhumiwa wanaozidi 600 aliachiwa huru na Mahakama, watuhumiwa wanaozidi 13,000 kesi zao zipo katika hatua mbalimbali za upelelezi,” alisema Mhe. Masauni.
“Mheshimiwa Naibu Spika kupitia bunge lako tukufu natoa wito kwa wananchi na wageni wanaojihusisha na biashara hii haramu kwa kuwa hakuna atakaebaki salama kwenye mapambano haya. Serikali kupitia vyombo vyake inaendelea kuwasaka wahusika wote ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria .”
No comments