Wanajeshi saba wa Marekani Kudhaniwa kupotea Baada Manuali ya Jeshi kugongana na Meli za Mizigo
Wanajeshi saba wanamaji wa Marekani hawajulikani waliko baada ya meli yao USS Fitzgerald, kugongana na meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Ufilipino, katika pwani ya mashariki mwa Japan.
Walinzi wa pwani ya Japan wametuma maboti tano na ndege mbili katika eneo hilo kusaidia katika shughuli za uokozi.
Msemaji wa jeshi la maji la Marekani, amesema huenda maafisa hao wako sehemu za ndani za zilizofungwa ili kuzuia maji zaidi kuingia ndani ya manuari hiyo.
Hakuna taarifa zozote zilizotolewa juu ya meli ya pili iliyokuwa na bendera ya Ufilipino ACX Crystal.
Meli hiyo ya kijeshi iligongwa na ile ya mizigo umbali wa kilomita 104 kusini magharibi mwa Yokosuka.
Haijulikani ni wapi meli hiyo ya urefu wa mita 154 ambayo ni ya kuharibu makombora ilikuwa ikielekea wakati huo.
eli ya mizingo ya ACX Crystal yenye urefu wa mita 222 iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Ufilipo ilikuwa ikisafiri kati ya miji ya Japan ya Nagoya na Tokyo.
No comments