China kujenga shule ya usafirishaji nchini
Balozi wa China nchini, Dk Lu Youging
Akizungumza leo (Jumamosi) katika hafla ya kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini iliyoandaliwa na taasisi ya Confucius, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youging amesema wakimaliza mazungumzo hayo wataanza ujenzi mara moja.
Dar es Salaam. Serikali ya China imesema kuwa ipo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania ya kujenga shule ya usafirishaji hapa nchini.
Akizungumza leo (Jumamosi) katika hafla ya kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini iliyoandaliwa na taasisi ya Confucius, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youging amesema wakimaliza mazungumzo hayo wataanza ujenzi mara moja.
Amesema lengo la ujenzi wa shule hiyo ni kuwaongezea ujuzi wahitimu na wale wasiokuwa wahitimu wa vyuo vikuu.
Amesema kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji wa China hapa nchini ni kiasi cha dola bilioni saba huku kampuni zaidi ya 1,000 zikifanya shughuli zake na kutoa ajira 1,200 kwa Watanzania.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo amezipongeza kampuni za China kwa kuisaidia Serikali kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira.
“Wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini wasiichukulie fursa hii kimzaha bali waifanyie kazi kuhakikisha wanakuwa na weledi tofauti na wengine,” amesema Samia na kuongeza:
"Lakini pia wanaposoma wajiandae kwa ajili ya kuajiriwa na kujiajiri, hivyo waongeze ubunifu binafsi kujitofautisha ili kuingia kwenye soko la kuajiriwa na kujiajiri."
No comments