Breaking News

Tanzania kunufaika na ujio wa timu ya Everton

Ushiriki wa kampuni ya michezo ya kubashiri (SportPesa) kwenye soka la Tanzania, umepongezwa na kuchukuliwa kama kichocheo cha msingi ambacho nchi ilikuwa inahitaji kuweza kuboresha sekta ya michezo nchini.

Katibu Mkuu Shirikisho la Soka Tanzania, Celestine Mwesigwa alisema kuwa wanaamini ushirikiano na kampuni hiyo itakuwa chachu ya muendelezo wa Soka hapa nchini kama ilivyofanikiwa nchi jirani ya Kenya ambayo imepanda daraja kutoka nafasi ya 99 hadi 74 katika viwango vya FIFA duniani.

“Soka la sasa limekuwa na gharama sana kulimudu hasa kwa nchi za Afrika. Inahitaji kuwa na fedha za kutosha ili kuweza kuendesha shughuli mbalimbali zinazohusiana na soka kutokana na mashirika mengi hayako tayari kuwekeza katika soka hivyo basi, anapopatikana mdhamini ambaye yuko tayari kufadhili shughuli za soka nchini basi huna budi kuonyesha shukrani zako za dhati” Mwesigwa alisema.

Aliongeza kwa kuwa “ mashindano ya SportPesa Super Cup ambapo timu ya Kenya imeongoza wapinzani wao Tanzania. Ni matumaini kuwa ni suala la muda tu kabla ya nchi kupata uzoefu zaidi kwenye swala zima la soka.”

Mwesigwa alibainisha matokeo ya kampuni ya michezo ya kubashiri Tanzania SportPesa ambayo ilianzishwa tarehe 9 Mei na tayari jitihada zimeanza kuonekana na na kutarajia kupanda daraja kutoka nafasi ya 139 katika vuiwango vya FIFA Duniani.

Mkuu wa Shirikisho anaamini kuwa Tanzania itaanza kupanda kwa kasi viwango vyake kutokana na ushirikiano uliotolewa na SportPesa ambao utahusisha timu za Tanzania (Simba, Yanga , Singida United na Serengeti Boys.

“Kenya imeweza kufaidika tangu kuanza kushirikiana na SportPesa kwenye soka nchini humo. Tunatarajia kitu kama hicho kutokea nchini kwetu maana tumeshaanza kuona baadhi ya ishara kwenye soka letu.

 Katika kuanza ushirikiano na soka la Tanzania shilingi milioni 50 zilitolewa kama mwanzo wa mahusiano na pesa za viingilio vya SportPesa Super Cup zitaelekezwa kwenye vilabu vya vijana chini ya miaka 13-15,” alisema Katibu Mkuu.”

“Kwa kipindi cha muda mfupi tangu kuingia kwao nchini, tumeshuhudia michango mbalimbali iliyotolewa na SportPesa nchini Tanzania.”

“Vilabu vya Soka nchini vimefaidika moja kwa moja kupitia SportPesa na tunaamini uhusiano walionao na vilabu vya soka Uingereza utaleta faida kubwa, Mwesingwa aliongeza”

Kwa mara ya tisa mfululizo mabingwa wa Ligi kuu Uingereza Everton watapata nafasi ya kufanya ziara nchini na kucheza na washindi wa SportPesa Super Cup 2017 nchini Tanzania.

Ziara hii inalengo la kujenga na kuendeleza miradi ya jamii kupitia soka nchini Tanzania, Pia timu hiyo inatarajia kuzindua miradi ya visima vya maji Tandale, Mbagala na Manzese kwa kushirikiana na SportPesa.

Uongozi wa Everton wamepanga kutembelea vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima na watu wenye ulemavu nchini Tanzania, pia wachezaji soka wamepewa mualiko wa kuhudhuria fainali na kupata nafasi ya kufahamiana na wageni wetu.

Sanjari na hayo SportPesa itashirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kutumia ujio wa timu ya Everton kukuza utalii Tanzania. Na kuwa kivutio nchini Uingereza ili kuvutia wageni kutoka Uingereza kukuza sekta ya utalii nchini.

Tanzania imewekwa miongoni mwa nchi zitakazonufaika na makambi ya mafunzo kwa timu, makocha , wachezaji vijana na pia safari za mafunzo nchini Uingereza.

SportPesa ni washirika wa vilabu vya soka kama vile Arsenal , Southampton , kutoka ligi kuu ya Uingereza , Hull City Tigers wa michuano ya Hispania ( LaLiga ) na kutoa mafunzo kwa viongozi wa mpira wa miguu nchini Tanzania.

 

No comments