Stamina, Darassa Kulipeleka Jiji Dar Live Sikukuu ya Idd Mosi
Rapper wa Morogoro, Stamina akifanya yake stejini.
SIKU zikiwa zinahesabika kufi kia Sikukuu ya Idd Mosi, wakali kibao wa michano wakiongozwa na R.O.M.A Mkatoliki,Stamina, Darassa, Moni na wengineo wanatarajia kulipeleka jiji ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar na kufanya makamuzi ya kihistoria katika bonge la shoo lijulikanalo kama Nishushe Dar Live.
Akizungumza na Uwazi Showbiz, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mara ya mwisho kwa R.O.M.A kufanya shoo ilikuwa Dar Live na safari hii anarudi akiwa mpya ndani ya uwanja huo akiwa na sapraizi kibao katika shoo kabambe inayotambulika kama Nishushe Dar Live.
“Tunajua kiu ya mashabiki wengi kumuona live R.O.M.A akikamua jukwaani na safari hii tena tumewaletea mtu wenu. Ni wakati kwa shabiki yeyote mpenda burudani kujitokeza na kukata kiu kwa shoo ya kihistoria ambayo ataliamsha dude msilolitegemea. “Kama mtakumbuka shoo yake hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya alikuwa katika michano mikali na msanii Darassa na mliona shughuli yake.
Msanii wa Bongo Fleva, Darassa.
Safari hii anashuka kuchukua kijiji chake na kuondoka nacho,” alisema Mbizo.
MSIKIE R.O.M.A MWENYEWE
“Sijawahi kuwaangusha mashabiki wangu tangu nimeanza muziki. Siku zote ni mzee wa kuondoka na kijiji. Nitadondosha ngoma zangu zote kali kama Viva Roma Viva, K, Ivan, Kaa Tayari na nyingine kibao kikubwa njoo wewe na yule tujumuike pamoja na kumshuhudia R.O.M.A mpya nikiwa na ngoma mpya kwa mara ya kwanza tangu mwaka uanze,” alisema R.O.M.A. MR. BLUE YUMO! Mbizo aliongeza kuwa mbali na uwepo wa R.O.M.A siku hiyo jukwaa litapambwa na wakali wengine kibao wakiongozwa na Mr.Blue. “Wote tunamjua Mr. Blue anayebamba na nyimbo kibao kama vile Pesa, Mboga Saba na Baki Na Mimi. Mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia amshaamsha ambalo halijawahi kutokea popote.”
Roma Mkatoliki akikinukisha
STAMINA WA MICHANO
Darassa Kuhusiana na mkali mwingine wa michano, Stamina, Mbizo alisema kuwa safari hii Dar Live imejiandaa kutoa burudani kwa mashabiki wake wote kwa kuangalia wanataka nini na kwa kipindi gani hivyo katika sikukuu hii Stamina atawapa kinachostahili.
“Stamina ni mmoja kati ya wakali wa michano wabishi na kila wakitoa ngoma huwa gumzo. Alishawahi kufanya michano na R.O.M.A katika shoo moja lakini hii ya safari hii itakuwa zaidi ya chana nikuchane kila mmoja akitambaa na biti la mwenzake,” alibonyeza Mbizo. Snura wa Chura Mbizo alimuongelea pia mkali wa nyimbo za mduara, Snura a.k.a Mamaa Chura au Mamaa Majanga kuwa atakuwa miongoni mwa wakata kiu kwa mashabiki wote watakaojitokeza Dar Live. “Chura zitakuwa za kumwaga na siku hiyo atakayepatia kucheza chura atapewa zawadi nono kutoka kwa Snura.”
Msanii wa Bongo Fleva, Snura.
ZANZIBAR STARS KUIBUKA
Baada ya kupotea kwa muda, kundi kongwe la Muziki wa Mwambao, Zanzibar Stars litaibuka kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live likiwa na vichwa hatari kama Bi. Mwanahawa, Sabaha Mchacho, Jokha Kassim, Mosi Suleiman, Ally Jay, Zubeda Mlamali na wengine kibao.
SHOO YA WATOTO SASA!
Mbizo aliongeza kuwa, mbali na shoo hizo pia pazia la burudani litafunguliwa Sikukuu ya Idd Mosi mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa kundi la sarakasi lisilo na mpinzani Bongo, Wakali Dancers pamoja na Makhirikhiri kutoka Tanzania pamoja na mchekeshaji anayebamba kunako kundi la Ze Comedy, Bambo ambao wataliamsha kwa kutoa burudani kwa watoto. “Kutakuwa na michezo mingi ya watoto kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea, kucheza ndani ya ndege na mingine mingi.”
MTONYO JE?
Mbizo alimaliza kwa kutaja kiingilio kwa siku hiyo kuwa, burudani kwa wakubwa itakayoanza saa 2:00 za usiku itakwenda kwa shilingi 7,000 huku watoto ikiwa kiduchu cha shilingi 3,000.
Download app ya masangulatz hapahttps://play.google.com/store/apps/details?id=com.masangula
JIUNGE NA MASANGULATZ.COM SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtubekuangalia video zote kali kutoka masangulatz blog
No comments