Sababu ya Mechi ya Taifa Stars Vs Lesotho kupigwa Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa
MCHEZO wa kwanza wa Kundi la kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji, Tanzania ‘Taifa Stars’ na Lesotho ‘Mamba’ utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, hamazi, Dar es Salaam Jumamosi kuanzia Saa 2:00 usiku.
Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
Malinzi amesema sababu za mchezo huo kufanyika Uwanja wa klabu ya Azam ni kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa katika matengenezo madogo.
Rais Malinzi amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumamosi Azam Complex, kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri.
Taifa Stars itaingiaa kwenye mchezo huo ikitoka kwenye kambi ya wiki moja mjini Alexandria, Misri.
Nahodha Mbwana Ally Samatta hakuwepo Misri na anatarajiwa kuungana na wenzake hapa Dar es Salaam akitokea Ubelgiji ambako anachezea klabu ya KRC Genk.
Kiungo wa DC Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa AFC Eskilstuna ya Denmark, Thomas Ulimwengu wao walikuwepo Misri na wako tayari kwa mchezo wa keshokutwa.
No comments