‘Nimewahi kucheza ‘Ndondo’ nikiwa Kenya’ – Wanyama
Leo Juni 24, 2017 michuano ya Ndondo Cup 2017 itaandika historia kwa kutembelewa na star wa ligi kuu ya England Victor Wanyama ambapo atashuhudia mechi ya Kundi H kati ya FC Kauzu dhidi ya Faru Jeuri kwenye uwanja wa Kinesi.
Wanyama amesema hata yeye pia amewahi kucheza Ndondo akiwa Kenya ambapo kwao wanaiita ‘Kothbiro’ ikiwa na maana ya msimu wa mvua.
“Kwetu pia kuna Ndondo sisi tunaiita ‘Kothbiro’ manaa yake ni msimu wa mvua, wanaocheza ni wachezaji wa mitaani na wachezaji wanaocheza ligi kuu wanachanganyika pamoja.”
“Kothbiro inanafasi kubwa Kenya kwa sababu imetoa wachezaji wakubwa na inasaidia timu za ligi kupata wachezaji kwa sababu makocha mbalimbali wa ligi huwa wanahudhuria kuangalia vipaji.”
“Mimi nimewahi kucheza Kothbiro na nilichezea timu yangu ya mtaani badae timu zikaanza kuwinda wachezaji mimi nikachukuliwa na timu inaitwa Ziwani.”
Wanyama amesema anatarajia kushuhudia mechi kali yenye ushindani kwa sababu ameambiwa timu hizo zilishawahi kukutana kwenye fainali ya michuano hiyo.
“Natarajia mechi safi kwa sababu nimesikia hizo timu zimewahi kucheza fainali kwa hiyo nadhani itakuwa ni mechi kali sana. “
Amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo na kuwa watulivu ili mechi imalizike kwa salama na amani.
“Mashabiki waje kwa wingi kushangilia timu zao na wasilete fujo iwe mechi ya amani.”
No comments