Mama Lulu Amaliza Bifu Na Mama Kanumba
DAR ES SALAAM: Baada ya kuwa katika mgogoro kwa muda mrefu, wazazi wa kike wa waigizaji marehemu Steven Kanumba naElizabeth Michael ‘Lulu’hatimaye wamemaliza bifu lao na hivi sasa, hakuna mwenye kinyongo tena. Wazazi hao, Lucresia Karugila wa Lulu na Flora Mtegoawa marehemu Kanumba, awali walikuwa mashoga wakubwa, kabla ya upepo kubadilika na baadaye kukosekana kwa maelewano baina yao. Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na wawili hao, hivi sasa wazazi hao wana mawasiliano kama ilivyokuwa zamani.
Lucresia Karugila mama mzazi wa Lulu.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mama mzazi wa Lulu ambaye baada ya kuulizwa kuhusu habari hizo njema, alikiri ni kweli wamerejea katika uhusiano wao kama zamani.
“Mimi sina ugomvi na mama Kanumba kabisa, niko naye vizuri, tatizo maneno ya watu ndiyo yanatuharibia,” alisema kwa kifupi.
Kwa upande wake, mama Kanumba alipotafutwa alijibu kwa kifupi tu; “Siku zote huwa nasema kila kinachotokea Mungu ameshapanga hivyo, sina tatizo na mama Lulu.”
No comments