Shilole aibiwa account yake ya Instagram
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amemlilia Mungu na kulaani vikali watu walioingilia akaunti yake katika Mtandao wa Instagram ambako huwa anaposti mambo yake mbalimbali ya kikazi.
Akizungumza na Za Motomoto News, Shilole alisema mpaka sasa wanaendelea kuishughulikia akaunti hiyo irudi na hana mpango wa kufungua nyingine ila waliofanya hivyo anawakabidhi kwa Mungu awafanyie kazi mwenyewe.
“Sifungui akaunti nyingine, bado tunaishughulikia hii maana watu wengi wanaijua na napata wateja wengine hasa kwenye biashara yangu ya chakula na shoo mbalimbali, hao walioiba nawakabidhi kwa Mungu,” alisema Shilole.
No comments