Breaking News

Kiporo cha majibu ya maaskofu sakata la mchanga leo

Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre, Askofu Onesmo Ngegi akimuuliza swali Rais John Magufuli kwenye hafla ya kupokea ripoti ya kamati maalum iliyokuwa ikichunguza kiwango cha madini yaliyomo kwenye mchanga uliopo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali sehemu mbalimbali hapa nchini, iliyofanyika Ikulu, Mei 24, mwaka huu. Picha na Maktaba

Viongozi hao, Padri Raymond Saba, ambaye ni katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Askofu Onesmo Ndege (Living Water) na Oscar Mnunga (Anglikana) waliuliza maswali tofauti wakati wa hafla, iliyoshereheshwa kwa burudani ya kukabidhi ripoti ya kwanza ya kamati iliyoundwa na Rais Magufuli kutathmini kiwango cha madini kilichomo katika makontena 277 yaliyozuiwa bandarini.

Kiporo cha maswali yaliyoulizwa na viongozi watatu wa dini kwa Rais John Magufuli kuhusu sakata la mchanga wa madini, likiwemo la kuchukulia hatua waliohusika, litajibiwa leo wakati kamati ya pili itakapowasilisha ripoti yake.

Viongozi hao, Padri Raymond Saba, ambaye ni katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Askofu Onesmo Ndege (Living Water) na Oscar Mnunga (Anglikana) waliuliza maswali tofauti wakati wa hafla, iliyoshereheshwa kwa burudani ya kukabidhi ripoti ya kwanza ya kamati iliyoundwa na Rais Magufuli kutathmini kiwango cha madini kilichomo katika makontena 277 yaliyozuiwa bandarini.

“Swali langu ni hawa waliohusika na mambo haya, ambayo yanatia uchungu na hasira, watashughulikiwa hawa wa mwaka huu au na wa miaka iliyopita,” aliuliza kiongozi huyo wa kidini, ambaye alikuwa wa mwisho kuuliza swali na hakutaja jina.

Hilo ni swali ambalo lilitaka moja ya majibu ambayo yamekuwa yakiulizwa muda mrefu bungeni na katika mijadala kuhusu udhaifu wa mikataba ya madini na tuhuma za kuweka mbele masilahi binafsi na hivyo kutaka wote waliohusika bila ya kujali nafasi zao wachukuliwe hatua.

Swali la kwanza katika hafla hiyo liliulizwa na Padri Saba, aliyetaka kujua idadi ya makontena yaliyosafirishwa nje tangu utaratibu huo uanze.

“Kama ni makontena tu mia mbili sabini na ngapi yaliyofanyiwa uchunguzi sasa na shughuli hiyo imekuwa ikifanyika kwa miaka mingi, sijui kama mnaweza mkatupa picha kwa miaka yote hiyo--labda katika takwimu hizo za (Wakala wa Ukaguzi wa Madini) TMAA-- ni makontena mangapi yaliyokwisha kutoka yakaenda huko, na labda hata upotevu ni kiasi gani kama mlifanya ukokotozi huo,” aliuliza Padri Saba.

Swali lililoulizwa na Askofu Ndege lilikuwa ni kuhusu thamani ya kujenga kinu cha kuyeyushia mchanga wa madini.

“Swali langu ni je, smelter haziuzwi? Hakuna mahali zinakouzwa hizo mashine zikanunuliwa na kuletwa hapa nchini?” alihoji.

“Na pili, kama wanasema bei ni kubwa, bei zake ni kubwa kuliko ndege tunazonunua mpaka tushindwe kuzinunua hizo mashine ikatusaidia hapa kuliko kupeleka hiyo michanga.”

Katika hotuba yake, Rais Magufuli alisema majibu ya maswali hayo yatapatikana baada ya kamati ya pili, inayohusisha wanasheria na wachumi, itakapotoa ripoti yake.

Kama ripoti hizo zitakuja na majibu ya swali la Askofu Mnunga, kuna uwezekano wa waliohusika katika mikataba hiyo wakachukuliwa hatua au wale wanaosimamia hivi sasa, kama ilivyokuwa kwa Profesa Sospeter Muhongo wakaadhibiwa.

Ripoti hiyo pia itajibu swali la uwezo wa kujenga kinu cha kuyeyushia mchanga baada ya ripoti iliyoundwa na TMAA kuonyesha kuwa kujenga mashine hiyo hakutawezekana kibiashara kwa kuwa mchanga unaozalishwa nchini ni asilimia 40 tu ya mahitaji.

No comments