Breaking News

Humphrey Polepole Sio Mtu wa Mchezo Mchezo..Adai CCM Kuna Minyoo na Kupe Wanaokiuwa Chama


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama wake kutowachagua viongozi wanaotafuna mali za chama hicho kwa maslahi binafsi.

Akizungumza na vijana wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam,

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole amesema leo (Jumapili) kuwa wako viongozi wa chama hicho wenye tabia ya minyoo na kupe.

"Wapigeni chini viongozi wenye tabia za kupe kwani ndiyo wanaokiua chama," amesema.

Amesema viongozi wa aina hiyo siku zao zinahesabika kwa kuwa wamesababisha wanachama kukichukia chama chao.
OK

No comments