Breaking News

Confederation Cup 2017: Chile na Ujerumani uso kwa uso fainali

Timu ya taifa ya Chile na Ujerumani zitakutana tena katika hatua ya fainali ya kombe la mabara katika ngazi ya timu za taifa (Confederation Cup) Jumapili hii.

Timu hizo zote ambazo ziliuwa katika kundi B, zilikutana katika hatua ya makundi na zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Goli la Chile lilifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 6 na Ujerumani walisawazisha kupitia kwa Lars Stindl dakika ya 41.

Chile walitinga katika hatua hiyo ya fainali usiku wa Jumatano hii kwa mara ya kwanza baada ya kuinyuka Ureno kwa mikwaju ya penati 3-0 baada ya kutoka sare ya kutofungana katika dakika 120 za mchezo huo.

Nao Ujerumani wametinga katika hatua hiyo baada ya hapo jana usiku kuicharaza bila huruma timu ya Mexico kwa mabao 4-1. Leon Goretzka (alifunga mabao mawili), Timo Werner, Amin Younes, na bao la kufutia machozi la Mexico lilifungwa na Marco Fabian dakika ya 89.

No comments