Breaking News

Kauli ya Godbless Lema kwa vijana

Mbunge Godbless Lema amefunguka na kutoa utabiri mwingine mpya kuwa katika nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kila nyumba itakuwa na watu waliomaliza shahada ya kwanza na 'masters' lakini hazitakuwa na tija katika maisha yao na nchi kwa ujumla. 

Godbless Lema amesema hayo alipokuwa katika mahafali ya Umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHASO) ambapo amewataka wanafunzi hao kuwa na maadili na maono katika maisha yao huku akisema hata katika vita ambayo nchi inapigana sasa, watu wanaoturudisha nyuma ni wasomi ambao wameshindwa kutambua wajibu wao. 

"Ambalo mimi naliona ni vijana wenye vyeti lakini hawana 'moral authority' nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kutoka sasa utakuta kila familia ina degree, kila familia ina masters lakini zisizona tija. Wasomi wasio na moral authority ni hatari kuliko wajinga wenye moral authority na hata ukiangalia kwenye haya mapambano wanaofanya kazi yetu inakuwa ngumu ni wasomi ambao wameshindwa kujua wajibu wao" alisema Godbless Lema 

Mbali na hilo Lema amesema wasomi wengi wa sasa ambao ni vijana wamekuwa ni watu wasiojali mambo ya msingi, wamekuwa wakijali sana mambo yasiyokuwa na tija katika nchi au taifa na kuikacha siasa ambayo ndiyo msingi wa kila kitu. 

"Vijana wa sasa hamjali mnajua mambo ya mipira, yaani vijana wasomi wa nchi hii wanajua zaidi mipira sijui 'Premier League' mimi siyajui vizuri hayo mambo, yaani 'commitment' yenu kwenye mambo ambayo hayawezi kuleta tija kwenye nchi imekuwa kubwa kuliko 'commitment' yenu kwenye mambo ya siasa" alisisitiza  Lema

No comments