Video: Hatutawaacha wanaoua Kibiti- Mwigulu Nchemba
May 22, 2017
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amesema Serikali haItawaacha wanaoua na wala haitawaacha wanaoshirikiana na wanaoua huku akisema umefika wakati watu waondokane na dhana kuwa wauaji wamekimbilia mahali pasipojulikana ilhali wapo hapo hapo Kibiti.
Akizungumza katika jiji cha Bungu, Kibiti ilipokambi ya Polisi wanaotunza amani, Mh. Nchemba amewataka polisi hao kusonga mbele katika mapambano ya kuwasaka wauaji.
“Hatutawaacha wanaoua na wala hatutawaacha wanaoshirikiana na wanaoua, hakuna chama cha siasa ambacho kina thamani sawa na maisha ya mwnadamu, kwa mujibu wa katiba yetu mtu yoyote mtu kuwa chama anachotaka hajafanya kosa hata kustahili kuuawa, hajafanya kosa, kwa hiyo kamaa hiyo mimi naona nikitafakari naona kuna kamchezo kanakochezwa”-Waziri Mwigulu
“Tusipoangalia kamchezo kanakochezwa, tutatafuta maadui ambao hawakuwepo na tutaacha maadui waliopo, tushughulike na adui aliyepo, tuwakamate wote wanaofanya vitendo hivi ,tusitafute adui kwa kuwaza hatuwezi kuruhusu ka Somalia au kaeneo kakipuuzi kama maeneo mengine yasiyoweza kutawalika katika nchi yetu ya Tanzania.”
No comments