Breaking News

Diamond kumtambulisha msanii mpya wa WCB leo

May 22/ 2017

Rais label ya WCB, Diamond Platnumz Jumatatu hii atamtambulisha msanii mpya wa label hiyo.

Msanii huyo atakuwa msanii wa 5 kutoka ndani wa label hiyo ambayo ina wasanii 4 akiwemo Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny pamoja na Queen Darleen.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Marry You, amesema anafanya hivyo ili kuwasaidia wasanii wachanga ambao wanavipaji lakini wanashindwa kufikia malengo yao.

“Panapo majaaliwa siku ya Jumatatu kesho (leo), ntakuwepo kwenye Leo tena ya Clouds Fm na familia nzima ya WCB Wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu mwingine mpya toka mtaani, ndani ya WCB,” aliandika Diamond Instagram.

Aliongeza, “Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake. Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha. Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran

No comments