Breaking News

Singida United yatumia busara za Mwl. Nyerere

Baada ya klabu ya Singida United kumruhusu mlinzi wake wa kati Elisha Muroiwa kwenda kwao Zimbambwe kushughulikia matatizo ya kifamilia kwa miezi tisa hatmaye Mkurugenzi wa timu hiyo Festo Sanga ameeleza sababu za kufanya hivyo. 
Akiongea na East Africa Television Sanga amesema kuwa wao kama timu hawkauangalia sana mkataba unasema nini kwani mchezaji naye ni binadamu na ana maisha nje ya soka.
''Ni kweli tulimruhusu mlinzi wetu na timu ya taifa ya Zimbambwe Elisha Muroiwa kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia tangu Disemba mwaka jana lakini sasa amerejea, tulitumia busara tu na hata Nyerere alisema sheria ikitumika sana tutashindwa kuendesha nchi'', - amesema.
Sanga pia ameongeza kuwa kipindi chote ambacho Muroiwa alikuwa kwao, walihakikisha anaendelea na mazoezi kwenye klabu ya Harare City Stars ambayo walimkabidhi ili asipoteze kiwango.
Muroiwa tayari amerejea nchini na ameshajiunga na timu hiyo ambayo ipo jijini Arusha tayari kwa maandalizi ya mchezo wa fainali ya Kombe la FA.

No comments