Mbao wataja sababu ya kufungwa na Yanga

Kocha
huyo amesema hayo Mei 22, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari
baaada ya kumalizika mchezo huo na kuongeza kuwa Habib Kiyombo ni
mchezaji muhimu na ndiye mfungaji bora katika timu ya Mbao kwahiyo
kukosekana kwake kumechangia timu hiyo kupoteza mchezo huo.
“Umuhimu wa Habib Kiyombo upo katika timu na ukizingatia yeye ndiye mfungaji bora katika timu yetu, kwahiyo kukosekana kwake kumepunguza kwa kiasi fulani asilimia za kushinda, lakini kingine ukiangalia katika mchezo wa kwanza yeye ndiye alitufungia magoli kwahiyo kutokuwepo kwake kumechangia sisi kupoteza nafasi za wazi ambazo tulizipata” amesema Fulgence
Kocha Fulgence ameongeza kuwa alijaribu kutumia wachezaji wengi wa kikosi cha pili katika mchezo huo lengo likiwa ni kuwapa uzoefu kwaajili ya maandalizi ya msimu wa ujao wa ligi na kutaka kuonesha ubora wa wachezaji hao ingawa walikuwa hawapati nafasi mara kwa mara.
Jana Mei 22, 2018, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, timu ya Yanga ilishinda bao 1-0 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, goli pekee lilifungwa na kiungo Thabani Kamusoko kwa mpira wa adhabu katika dakika ya 26 na hivyo kuifanya klabu hiyo kufikisha alama 51 na kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi.

No comments