Mzee wa Upako Ampigia Simu Q-Chief ,Ni Baada ya Kusikia Anaacha Muziki.
Baada
ya kuweka wazi dhamira yake ya kuacha muziki, msanii Q Chief amesema
amepigiwa simu na watu wengi mmoja wapo ni Mchungaji Anthony Lusekelo
‘Mzee wa Upako’
Muimbaji huyo amesema kuwa Mzee wa Mpako alionyesha kuguswa na hatua hiyo aliyoamua kuichukua.
“Nimepokea
simu kutoka kwa mtu kama Anthony Lusekelo, usiku saa tisa, unaweza
kuona ni jinsi gani mchungaji anaweza kuguswa na kusema mwanangu
nimetaka kama kulia hivi, nimepigiwa simu na maostadhi wakubwa sana
Tanzania hii,” Q Chief ameiambia Clouds TV.
Ameongeza
kuwa amefikia maamuzi hayo na hana kinyongo chochote na mtu ila kwa
sasa ameona mapenzi makubwa sana kutoka kwa watu kwenda kwa Q Cheif.
No comments