Tanzania yalaani kauli ya Chief Rabbi kwa Waafrika
Kamati ya Mshikamano wa Tanzania na Palestina imelaani vikali matusi yaliyotamkwa na mkuu wa dini ya Wayahudi nchini Israel, Chief Rabbi Yitzhak Yosef ambaye, wakati wa mahubiri aliwafananisha Waafrika na kima.
Yosef ni mmoja kati ya wachungaji wawili wakuu wanaoteuliwa na serikali ya Israel. Alipokuwa akihubiri katika hekalu la Kiyahudi hivi majuzi aliwazungumzia Waafrika na akatumia neno “kushi” ambalo katika lugha ya Kiibrania ina maana ya “kima” .
Katika taarifa ya kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mwenyekiti Abdullah Othman imeeleza kuwa hiyo si mara ya kwanza kwa mchungaji huyu mkuu wa Israel kutumia maneno ya kuwadhalilisha Waafrika.
Othamn amesema katika mahubiri yake ya Mei mwaka jana alisema wanawake wana tabia ya wanyama kwa sababu ya mavazi yao huku mnamo Machi 2016 alitangaza kuwa watu wasio Wayahudi hawapaswi kuishi nchini Israeli.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa tayari onyo limetolewa kuwa kuanzia tarehe 1 Aprili 2018 kama Waafrika hao hawataondoka basi watakamatwa na kufungwa gerezani bila kikomo Israel imetangaza kuwa Waafrika wanaoishi ni tishio kwa utambulisho wa Kiyahudi.
Amesema kuwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyau amekuwa akitaka wafukuzwe na kusema kuwepo kwao nchini Israel ni tishio kwa “amani na usalama”.
No comments