Breaking News

RATIBA YA LEO JUMAPILI YA APRIL 08-2018 LIGI KUU TANZANIA BARA


RATIBA YA LEO JUMAPILI YA APRIL 08-2018 LIGI KUU TANZANIA BARA

Ligi kuu Tanzania Bara raundi ya 23 inatarajiwa kuendelea leo Jumapili ya Aprili 8-2018 kwa jumla ya michezo minne.

Mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Mbeya City watakaokuwa nyumbani kwenye uwanja wa kumbukumbu ya sokoine Jijini Mbeya kuwakaribisha mabingwa mara moja wa taji hilo, Azam FC saa 16:00 jioni.

Wapiga debe wa Shinyanga timu soka ya Stand United maarufu kama ‘chama la wana’ wao watakuwa nyumbani katika dimba la CCM Kambarage kucheza na Njombe Mji saa 16:00 jioni.

Ndanda FC wao watawakaribisha wanankurukumbi Kagera Sugar katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara saa 16:00 jioni.

Mchezo wa mwisho kwa wikiend hii ya raundi ya 23 utakuwa kati ya Wafunga buti Ruvu Shooting dhidi ya Wajelajela Tanzania Prisons katika uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani saa 16:00 jioni.

No comments