Breaking News

HUYU JOSEE MOURINHO AISHIWI MANENO


MOURINHO ANAPOBAKI MTAALAMU WA MBINU.

Linapokuja swala la mbinu bado sioni mtu anaeweza kulimudu hili kwa ufasaha kama Jose Mourinho. Kimsingi anaweza kuwa na mpira usiovutia na wakujihami lakini kupitia mbinu zake, Manchester United wamekuwa na ubavu wa kupata matokeo msimu huu dhidi ya timu kubwa hata ugenini dhidi ya Manchester City leo na Arsenal kwenye mzunguko wa kwanza mwaka jana pale Emirates.

Ligi kuu England imeleta pamoja makocha sita bora zaidi kwenye ligi hiyo kwa misimu miwili sasa lakini linapokuja swala la mbinu miamba hao wa kufundisha soka wanapokutana basi Mourinho huwa ni level nyingine.

Huo huo mpira wake usiovutia wakati mwingine ndipo anapochanganya na mbinu zake na matokeo huwa yanakuja. Wanaweza kushikwa zaidi United lakini mwisho wa siku wao ndio huwa wanamaliza na matokeo yakiwa upande wao.

Siku zote Mourinho huwa anaonesha umwamba pale ambapo wengi huwa hawatarajii kumwona akifanya hivyo. Kwa ubora wa wapinzani wake msimu huu na itikadi yake ya kucheza soka la kujihami na uoga ni rahisi kuamini kuwa Mourinho anaweza kuwa ni mwathirika mkubwa dhidi ya timu za top 6 lakini Mourinho huwa ana mbinu madhubuti zaidi kufanya kweli licha ya kwamba wakati mwengine huwa zinakataa lakini leo mbinu zake zilibeba roho nyingi kwenye vitabu vya kumbukumbu na historia.

City wanahitaji kusubiri wiki nyingine moja kutwaa ubingwa wao lakini United wanatamba mbele ya hasimu na rekodi yake ya kutopoteza mara mbili dhidi ya timu moja inasimama kama ilivyo. Baada ya kipindi cha kwanza kibovu unaweza kudhani kuwa mwisho wa shoo ni aibu kwao lakini kwa mara nyingine tena Mourinho ameonesha kuwa yeye ni mtaalamu wa mbinu.

Kwanza aliituma timu iingie kwa presha kwenye kipindi cha pili na kuitia presha pia defence ya City na Paul Pogba akatumwa amalize kazi. Kitendo cha kupata bao la kwanza kilimaanisha kuwa nguvu yote ikahamia kwa upande wa United na si ajabu la pili halikuwa mbali.

Paul Pogba mara baada ya kufunga bao la kwanza bado akawa anaingia kwenye nafasi ya ushambuliaji na hichi kitendo kiliwachanganya mabeki wa City kwani hawakuwa wakitegemea kuwa Pogba anaweza kurudia mchezo ule. Tena baada ya hapo ndipo Paul akatuliza presha na kurudi kwenye nafasi yake lakini akili ilikuwa ni kwamba yule atakaefunga bao la kwanza aendelee kutia presha na kuingia kwenye nafasi ile ambayo kimsingi sio yake na mabeki wa City hawatotarajia na kufunga jingine.

Unaweza kuona kuwa pasi ya Pogba baada ya kuturn pale kati alikuwa anaweza kusimama na kumwacha Sanchez atembee lakini akajua kuwa goli lilishawachanganya City na yeye kwa mara nyingine hawakutegemea kumwona akiingia kwenye 18 yao lakini Pogba baada ya kuachia moja kwa Sanchez akaendelea kukimbia na Sanchez kwa kugundua kuwa mwenzie tayari ameingia ndani kutafuta kitu akaunyanyua mpira na Pogba hakufanya makosa. Hata baada ya hapo Pogba akatuliza presha, United wakarudi kwenye shepu yao na mbinu nyingine zikafuatia.

Wakati Sanchez anapiga faulo ya bao la Smalling unaweza kumwona akishinikiza wenzie kuingia Kati kwa ishara ya mikono. Kimsingi wachezaji wengi wa City hawakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuuokoa mpira ule kwa sababu walikuwa nje ya eneo la hatari na mpira uliingizwa ndani ya eneo hilo na ndipo Sanchez alipoashiria watu waingie wakakutane nao na Smalling akafunga bao akiwa peke yake na isitoshe kukiwa na wachezaji wengine wa United nyuma yake wakimfuatia.

Na ofcourse mabadiliko ya Rashford yalikuwa ni ya kutafuta mtu wa kukimbiza wakati United wako nyuma, McTominay ilikuwa ni kutuliza presha pale kati baada ya City kuja juu na Lindeloef ni kupoteza muda na mwisho wa siku yote hii ilikuwa ni mipango tu kutokana na mbinu za Mourinho. Yeye pia alikuwa anaijua athari ya kupoteza mechi hii. Mbinu za Mourinho zimemtoa mbali sana hakuwa na soka zuri tangu lakini mbinu hatari

Credit Haatim Abdul

No comments