Ndugai: Kanuni zinamtaka Bashe aipeleke hoja yake kwenye Chama chake kabla ya kuileta bungeni
Spika Job Ndugai akiongea kwa mara ya kwanza na mtangazaji Charls Hillary tangu arejee kutoka India kwa matibabu ameongelea suala la mbunge wa Nzega, Hussein Bashe kutoa hoja binafsi.
Amesema pamoja na Kanuni za Bunge pia zipo Kanuni za uendeshaji wa shughuli za Bunge kwa wabunge wa CCM kama chama tawala na zipo kama hizo kwa wabunge wa kambi ya upinzani ambazo zote ni sehemu ya uendeshaji wa shughuli za Bunge.
Amesema Bashe kama mbunge wa CCM, kanuni za wabunge wa CCM zinamtaka aipeleke hoja yake kwenye chama chake kwanza, ikajadiliwe huko na ikikubaliwa Bunge liweze kuipokea.
Ndugai amesema Bunge bado halijapokea hoja hiyo kutoka kwa Bashe pia halijapokea taarifa kutoka kwa katibu wa wabunge wa CCM kama wameipokea hoja hiyo na wameshaurianaje.
Kuhusu afya yake, amesema imeimarika ukilinganisha na miezi michache nyuma.
Hivi karibuni Mbunge Hussein Bashe (Nzega - CCM) alisema amemuandikia barua Katibu wa Bunge kuhusu ombi la kuwasilisha hoja binafsi bungeni ya kutaka kuundwa tume teule itakayochunguza matukio ya kihalifu nchini.
==>Msikilize hapo chini akiongea
No comments