Breaking News

Maulid Mtulia , Dk Godwin Mollel Waapishwa Bungenii Leo

Naibu Spika, Tulia Ackson, leo amewaapisha wabunge wawili, Dk Godwin Mollel wa Siha na Maulid Mtulia wa Kinondoni, leo Aprili 3.

Wabunge hao wameapishwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha na Kinondoni,  baada ya wabunge wa maeneo hayo kuhamia CCM.

Mtulia, alikuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena jimbo hilo kwa kupitia CCM.

 Kadhalika Mollel, alikuwa mbunge wa Siha, (Chadema) kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.

Hata hivyo kiapo hicho hakikushuhudiwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ambao hawakuwepo katika kikao cha leo.

 Hili ni bunge la kumi na moja na mkutano wa kumi na moja.

No comments