Breaking News

Goli la Okwi Lawapa Ushindi Simba Dhidi ya Mtibwa Sugar


Simba SC imeendelea kujikusanyia alama katika Ligi Kuu Bara baada ya kuilaza Mtibwa Sugar FC kwa bao 1-0 jioni hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezo huo uliokuwa unaambatana na mvua iliyokuwa ikinyesha Uwanjani, ulishuhudiwa nyavu zikitikiswa mnamo dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza na Emmanuel Okwi.
Okwi alifunga bao hilo akimalizia kazi mpira wa kichwa kutoka kwa John Bocco na kufanya mchezo huo udumu kwa dakika zote 90 huku matokeo yakisalia kuwa 1-0.
Matokeo hayo yanaifanya Simba izidi kujikita kileleni kwa kufikisha alama 52 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga wenye 46 mpaka sasa.
Mechi inayofuatia kwa Simba itakuwa dhidi ya Wajelajela Mbeya City FC, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Goli hili hapa

No comments