DANTE NJE KESHO WAKATI YANGA IKIVAA SINGIDA UNITED
Kikosi cha Yanga kinashuka Dimbani Taifa kesho Jumatano kikiwakaribisha walima alizeti, Singida United kutoka Singida katika mchezo wa ligi kuu bara.
Yanga itakuwa kibaruani ikiwa na kumbukumbu ya kuondoshwa na Singida kwa changamoto ya mikwaju ya penati kwenye michuano ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Namfua.
Kuelekea mchezo huo, Yanga itamkosa beki wake Andrew Vincent 'Dante' aliyeumia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaitta Dicha SC.
Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni.
No comments