Breaking News

BREAKING NEWS:MADIWANI, WAKILI, VIONGOZI NA WANACHAMA WA ACT WAZALENDO WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI

Mjumbe wa Kamati Kuu, na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Sheria ya ACT Wazalendo, Wakili Thomas Msasa Amekamatwa na polisi jana mjini Kigoma kwa sababu ya kuwatetea Madiwani, Viongozi na Wanachama wa Chama hicho waliokuwa wamekamatwa na Jeshi la Polisi jana.

Wakili Msasa alikwenda polisi kama Wakili wa Madiwani wawili wa ACT Wazalendo, Diwani wa Kata ya Kipampa, ndugu Mussa Mgongolwa, pamoja na Diwani wa Kata ya Kigoma, ndugu Hussein Kalyango, aliyekuwa mgombea Udiwani Kata ya Mwanga, ndugu Winston Mogha, Katibu wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Mkoa, ndugu Masabo, pamoja na wanachama na wafuasi mbalimbali wa ACT Wazalendo wa Mkoa wa Kigoma.

Kukamatwa huku ni sehemu ya mpango wa CCM na Jeshi la Polisi wa kukamata Viongozi na Wafuasi wa Vyama vya Upinzani unaoendelea nchi nzima, na kuhakikisha kuwa wanawaweka ndani kwa muda mrefu kwa uonevu tu.

Chama ngazi ya Mkoa, pamoja na Taifa tunashirikiana kuhakikisha wote waliokamatwa wanaachiwa au wanafikishwa mahakamani.

Sendwe Ibrahimu Mbaruku 
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Mkoa wa Kigoma
Aprili 1, 2018

No comments