Asilimia 5.8 ya Watanzania ni walemavu
Tanzania ina jumla ya watu wenye ulemavu 2,641,802 sawa na asilimia 5.8 ya wananchi wote.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa ameliambia Bunge leo Jumatano Aprili 11, 2018 kuwa idadi hiyo inabainishwa kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ambayo ilijumuisha vipengele vya kuwatambua wenye ulemavu.
Amesema ulemavu umegawanyika katika makundi mbalimbali ambapo wenye ulemavu wa ngozi wapo 16,477 (0.04), wasioona 848,530 (1.19).
Amebainisha kuwa wasiosikia wapo 425,322 (0.97), wasioweza kutembea 525,019 (1.19), wanaopoteza kumbukumbu ni 401,931 (0.91).
Amesema idadi ya watu ambao hawawezi kabisa kujihudumia ni 324,725 (0.74), ulemavu mwingine ni 99,798 (0.23).
Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Khadija Nassiri Ali ambaye alitaka kujua Serikali kama inajua idadi kamili ya watu wenye ulemavu waliokuwa nao.
No comments