Breaking News

ULIISIKIA HII YA SIMBA KUKATIWA RUFAA?,0 HAJI MANARA ANATOA UFAFANUZI


 Moja kati ya habari zilizoenea katika mitandao ya kijamii baada ya club ya Simba kufanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika CAF kwa kuitoa Gendermarie ya Djibout kwa jumla ya magoli 5-0.

Baada ya kufuzu kulianza minong’ono kuwa Gendermarie kama wakikata rufaa dhidi ya Simba, basi Simba watatolewa kutokana na kufanya udanganyifu kutokana na kumtumia mchezaji Paul Bukaba ambaye ni raia wa Burundi lakini ameandikwa kama mtanzania.


Haji Manara ametoa amefafanua kuhusiana na stori hizo na kusema kuwa Bukaba ni mtanzania “Tunazo taarifa za hovyo zinazosambazwa eti mchezaji wetu huyo ni Mrundi na hIvyo tutakatiwa rufaa dhidi ya Wadjibout.. Poul Bukaba @bukaba_paul ni mtanzania na Urundi alienda kucheza Soka tu”


“Anamiliki uraia wa kuzaliwa wa Tanzania…tafuteni lingine hili mmenoa na pia hangaikeni na yenu ikiwemo kulipa mishahara ya wachezaji wenu….Ndegelec”

No comments