Breaking News

REKODI MPYA ALIYOWEKA MESSI

NYOTA wa Klabu ya Barcelona na Timu yaTaifa ya Argentina, Lionel Messiamevunjarekodi ya kutofunga goli lolote dhidi ya Chelsea ya Uingereza pindi timu hizozinapokutana.

Imemchukua mchezaji kutumia dakika 730 namechi 9 kufunga bao lake la kwanza katikamichuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya(UEFA), ikiwa ni dakika ya 75 ya mchezousiku wa kuamkia leo.

Messi ambaye amekuwa yuko katika kikosi kimoja na Andres Iniesta tangu aanze kuichezea Barcelona, alikuwa hajawahi kuzitikisa nyavu za Chelsea hata mara moja.

Iniesta ndiye alimsaidia Messi kufunga bao hilo kwa pasi safi ikitokea upande wa kushoto mwa uwanja wa Stamford Bridge na kuizamisha nyavuni fasta.

Bao lake la kusawazisha limekuwa muhimu kwa Barcelona ambayo imekuwa na faida ya goli moja la ugenini, kabla timu hizo hazijakutana tena katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Camp Nou, Jumatano ya Machi 14, 2018.

No comments