TANZANIA NA MSUMBIJI KUBADILIHSANA UZOEFU WA GESI NA MAFUTA
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. FilipeJacinto Nyusi amefanya ziara ya kikazi yasiku moja hapa nchini ambapo amekutana nakufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Mjini Dodoma.
Mhe. Filipe Jacinto Nyusi amepokelewakatika uwanja wa ndege wa Dodoma namwenyeji wake Mhe. Rais Magufulialiyeongozana na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa na kisha viongozihao wamefanya mazungumzo rasmi nakusalimu wananchi kupitia vyombo vyahabari.
Mhe. Rais Nyusi amemshukuru Mhe. RaisMagufuli kwa kumpokea na kufanya naemazungumzo na amesema ujio wakeumelenga kuimarisha na kukuza zaidiuhusiano na ushirikiano wa kihistoria nakidugu kati ya nchi yake na Tanzania.
“Mhe. Rais Magufuli japo kuwa nimetoataarifa ya muda mfupi kuwa nakuja kuonananawe, umenikaribisha umenipokea natumezungumza mambo yenye manufaa kwanchi zetu, nakushukuru sana” amesema Mhe.Rais Nyusi.
Amebainisha kuwa yeye na Rais Magufuliwamezungumzia namna Tanzania naMsumbiji zitakavyobadilishana uzoefukuhusu ugunduzi mkubwa wa gesi na mafutauliofanikiwa katika nchi hizi, masuala yaulinzi na usalama na uimarishaji wamiundombinu ya usafiri.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuliamemshukuru Mhe. Rais Nyusi kwa kujaMjini Dodoma na kwa kudumisha uhusiano naushirikiano wa kidugu na kihistoriauliojengwa na waasisi wa mataifa haya HayatiBaba wa Taifa Mwl. Julius KambarageNyerere na Hayati Samora Machel waMsumbiji.
Mhe. Rais Magufuli amesema katikamazungumzo hayo pia wamekubaliana Tumeya pamoja ya ushirikiano ya Tanzania naMsumbiji zikutane haraka ili kuimarishamaeneo yote ya ushirikiano kwa manufaa yanchi hizo.
“Nafurahi kuwa Mhe. Rais Nyusi piaamesema Msumbiji itatoa kibali kwa Shirikala Ndege la Tanzania (ATCL) kufanya safari za moja kwa moja kati ya Tanzania naMsumbiji haraka iwezekanavyo, ili kurahisisha usafiri kati yetu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Nyusi ameondoka nchini jana jioni na kurejea nchini Msumbiji.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
No comments